Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kufanya uchunguzi wa uchenjuaji wa madini kinyume cha sheria kwa mkazi wa Wilaya ya Kahama Bw. Renatus Kanyali (36), huku akiwataka wananchi kuwafichua wale wote wanaofanya biashara hiyo kwenye makazi ya watu.
Mhe. Telack ametoa agizo hilo mapema jana baada ya kufanya ziara akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na kukuta mtambo wa kuzalisha mchanga aina ya “carbon” nyumbani kwa mkazi huyo kitu ambacho ni kinyume cha sheria ya madini ya mwaka 2010 kifungu cha 6.
Mkazi huyo anatuhumiwa kufanya shughuli ya kuchenjua madini kwa muda mrefu nyumbani kwake ambapo Ofisi ya madini Kanda na Wilaya ilishamzuia na kumfikisha Polisi, hivyo TAKUKURU ifuatilie kujua kwa sababu gani mkazi huyo ameweza kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu.
“Kifungu cha 6, 1-3 inasema kuwa mtu yeyote anayefanya shughuli za madini bila kibali faini mil.10 na kutaifishwa mali” amesema Mhe. Telack.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa imefika katika kituo cha Polisi Wilaya ya Kahama na kukuta kiasi ya kg 400 za mchanga zikiwa nje ya kituo na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo amepewa dhamana kinyume na utaratibu ambapo Mkuu wa Kituo hicho ameagizwa kuhakikisha mashitaka halali yanafunguliwa dhidi ya mtuhumiwa na anapelekwa mahakamani.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa