Na. Shinyanga RS
WANANCHI wa Kata ya Kinaga katika Manispaa ya Kahama mkoani shinyanga wamemshukuru sana Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Kituo cha Afya Kinaga chenye gharama
Zaidi ya wakazi 22,343 wa Kata ya Kinaga na vijiji jirani kunufaika na uwepo wa Kituo cha Afya Kinaga kilichopo Kata ya Kinaga, Manispaa ya Kahama kilichogharimu zaidi ya Tzs. Milioni 669 chanzo cha fedha ni serikali kuu Mil. 500 na Manispaa ya Kahama Mil. 169 kutoka mapato yake ya ndani.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata ya kinaga, Diwani Mhe. Mary Joseph Manyambo alisema kuwa, awali wananchi wa kata hii walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya Kilomita 15 kwenda Kahama mjini kufuata huduma ya afya ambapo hivi sasa wanapata hapahapa kinaga, hivyo wanamshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha aa ujenzi wa kituo hiki cha afya ambacho kimekuja kuwa mkombozi.
"Tunamshukukuru sana Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa kituo hiki, na leo wananchi wa kinaga wanapata huduma zote muhimu hapahapa kinaga," akisema Mhe. Mary.
Kwa upande wake DC wa Kahama Mhe. Mboni Mhita alimshukuru pia Rais. Mhw. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali wananchi hasa wa kahama ambapo leo wameshuhudia kufunguliwa rasmi kwa kituo cha afya, huku akiwataka wananchi kukitunza na kuwapa ushirkiano qahudumu wa afya kituoni hapo.
Akitoa salamu za mkoa, RC Mndeme amemshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zite hizi ili kuwajengea Kituo hiki na akawashukuru pia manispaa ya kahama kwa kujazia zaidi ya Mil 169 hivyo zaidi ya milioni 669 kugharamia ujenzi huu unaotarajiwa kukamilika Desemba 31, 2023.
Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi mganga mfawidhi kituo cha afya kinaga Bi. Maria Chaeka alisema, kukamilika kwa kituo hiki kunakwwenda kuwanufaisha wananchi 22,243 wa kata ya kinaga na vijiji jirani ambapo kituo kinajumuisha majengo ya wangonjwa wa nje (OPD), wodi ya kujifungulia akina mama wajawazito, upasuaji, maabara, kichomea taka, kitengo maalumu cha VVU, kifua kikuu pamoja na kkiniki ya baba, mama na mtoto.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa