Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewataka wakulima kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa kudhibiti panya waharibifu mashambani kwa ajili ya usalama wao na mifugo yao.
Mhe. Telack ametoa agizo hilo mapema leo tarehe 03/01/2019 akiwa katika kijiji cha Mwalata, kata ya Shagihilu, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakati wataalamu hao wakitoa Elimu ya utegaji wa panya hao kwa wakulima.
Amewahimiza viongozi na watendaji kuhakikisha wanatoa matangazo kwa wananchi kutopeleka mifugo mashambani hasa katika maeneo sumu hiyo itakapowekwa ili kuwanusuru na athari zake.
Akitoa elimu hiyo kwa wakulima, Afisa Kilimo kutoka kituo cha kudhibiti baa la panya Bw. Mathias Mchukya amesema sumu hiyo ni hatari kwa binadamu na mifugo hivyo iwekwe mbali na maeneo ya watu na itumike kwa ajili ya panya wa mashambani tu.
Amesema pia jumla ya Halmashauri 32 nchini zimekumbwa na tatizo la panya waharibifu.
Akitoa taarifa ya uharibifu wa panya hao katika Wilaya ya Kishapu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Shadrack Kengese amesema jumla ya kata 7 zimeathirika na tatizo hilo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa