Na. Shinyanga RS.
WAKUFUNZI wa mfumo mpya wa ununuzi NeST kutoka Ofisi ya Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 13 Septemba, 2023 wameanza mafunzo ya mfumo huo kwa wataalam wa Ofisi ya Shinyanga RS na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwapatia uelewa wa matumizi ya mfumo huo unaotajwa kuwa ni mwarobaini wa urasimu na ucheleweshaji katika mchakato wa kupata na kutoa huduma ya zabuni kwa wadau katika nyanja zote.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Kitengo cha Ugavi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ndg.Gervas Lugodisha na Ammy Mohmed ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wamewaeleza washiriki wa mafunzo haya kuwa Serikali imekuja na mfumo huu na kwamba sasa wataalam wanapaswa kuhama kutoka TANePS ule wa awali.
Wakufunzi wamesema kuwa awali Serikali ilikuwa ikitumia mfumo wa TANePS katika ununuzi wa Umma ambao ulibainika kuwa na changamoto, jambo ambalo lilipelekea Serikali kuja na mfumo huu wa NeST ili kuondoa changamoto hizo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma na kujikita katika matumizi ya Tehama zaidi.
Mfumo huu wa TANePS utafika ukomo wake rasmi ifikapo Septemba 30, 2023 na hivyo kutoa fursa kwa mfumo huu mpya wa NeST kuanza kutumika rasmi Octoba 1, 2023.
Aidha Taasisi hazitaruhusiwa kufanya ununuzi wowote wa umma nje ya mfumo huu mpya wa NeST, na kwamba Taasisi nunuzi ambayo itafanya ununuzi wowote bila kutumia mfumo wa NeST itakua imetenda kosa na hivyo Afisa Masuhuli wa Taasisi husika atachukuliwa hatua zinazostahili kwa mujibu wa Sheria.
Picha zikionesha baadhi ya washiriki wa mafunzo pamoja na wakufunzi wakiendelea na mafunzo ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Ndg. Gervas Lugodisha Mkufunzi na Mkuu wa Kitengo cha Ugavi Shinyanga RS.
Ndg. Ammy Mohmed Mkufunzi na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Shinyanga RS.
Picha za washiriki wakati wa mafunzo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa