Na. Paul Kasembo, SHY RS.
UONGOZI wa National Microfinance Bank (NMB) kutoka Makao Makuu ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Ruth Zaipuna wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanĝa Mhe. Anamringi Macha ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha ambapo pia wamepata wasaa wa kujadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ambavyo NMB wamejipanga kimkakati ili kuhakikisha wanawaingiza Watanzania katika Sekta ya NMB.
Akitoa salamu za Taasisi yao Bi. Ruth amesema kuwa, hivi sasa wamerahisisha zaidi huduma zao ambapo mwananchi anaweza kufungua akaunti yake hata kwa Tzs. 100 tu na kaanza kupata huduma huku akisisitiza kuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ni muhimu sana katika kuhakikisha NMB inaendelea kuwafikia Wanashinyanga.
Kwa upande wake RC Macha amewapongeza sana NMB kwa kuendelea kuwahudumia wananchi na kwamba ofisi yake itaendelea kushirikiana nao wakati wote ili kuhakikisha kuwa uchumi wa wanashinyanga unaimarika huku akiwakumbusha kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa