• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI IPO TAYARI KUIFANYA SHYCOM ALUMNI MARATHON KUWA YA KIMATAIFA- RC MACHA.

Posted on: September 21st, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa Serikali ipo tayari kuahirikiana na Uongozi wa Shycom Alumni Marathon 2024 na kuyafanya mashindano haya kuwa ya Kimataifa ambapo itaweza kuitangaza vema SHYCOM yenyewe, Shinyanga na Tanzania kwa ujumla kwani itajumlisha wakimbiaji kutoka ndani na nje ya Nchi pia.

Shycom Alumni Marathon 2024 ni mbio za hisani  ambao zimeandaliwa na waliokuwa wanafunzi wa Chuo hicho ambacho awali kilikuwa Chuo cha Biashara na sasa ni Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM)

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 21 Septemba, 2024 baada ya kukamilika kwa mbio hizi za hisani ambazo zimejumuisha wakimbiaji wa Kilometa 5, 10 na 21 na kisha kufungua mashindano ya mbio za baiskeli huku yeye RC Macha na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni wakishirki mbio za Kilometa 5 ambapo pia ametumia nafasi hii kuwapongeza wandaaji wote wa michezo hii na kusisitiza kuwa uwepo wa tukio hili hapa mjini limeongeza mzunguko wa fedha.

"Kupitia mbio hizi za hisani kuwa, Serikali inatambua na kuthamini sana uwepo wa michezo kwa wananchi wake, na hivyo niseme tu kwamba Serikali ipo tayari kushirikiana na Uongozi wa Shycom Alumni Marathon ili kuyafanya mashindano haya kuwa ya Kimataifa jambo ambalo litaitangaza vema Shyco, Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla," amesema RC Macha.

Akizungumza na wanahabari mlezi wa mashindano haya ambaye pia ni mmoja wa wanafunzi waliosoma Shycom Prof. Mussa Assad amesema kuwa uwepo wa Shycom Alumni Marathon hapa mkoani Shinyanga ni kukienzi Chuo, kukusanya fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Chuo hiki na kuwezesha wanachuo wengine kuendelea kunufaika na Chuo hiki ambacho kimekuwa na tija kubwa wa wengi zaidi.

SHYCOM ni Chuo ambacho kimetoa hazina kubwa ya wasomi hapa nchini akiwamo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hhesabu za Serikali (CAG), Profes Charles Kichere,  Prof Mussa Assad na wengine wengi zaidi kama walivyojitokeza leo huku wakitajwa kwa kuonesha uzalendo, wenye kujitoa na mfano wa kuigwa na wengine ambao wanaweza kurejesha fadhira kwa shule na vyuo walivyosoma.



Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • NATOA WITO KWA VIJANA HAPA SHINYANGA KUREJEA NA KUTATHIMINI UPYA NJIA ZA KUJIPATIA KIPATO - RC. MACHA

    May 20, 2025
  • SERIKALI YATHIBITISHA VIFO VYA WATU SITA NA MAJERUHI 11 KATIKA AJALI YA MGODI WA MWAKITOLYO.

    May 18, 2025
  • WAZAZI NA WALEZI, NENDENI MKAWE MABALOZI SAHIHI WA KAZI ZA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – RC. MACHA

    May 16, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa