RC MNDEME AWATAKA WANAFUNZI KUKATAA UKATILI
Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka wanafunzi kukataa ukatili wa aina yoyote na wakiona kuna viashiria vyovyote vya kufanyiwa ukatili watoe taarifa kwa wazazi, walezi, walimu, viongozi wa Serikali au katika ofisi yoyote ili mtu huyo aweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 19 Julai, 2023 wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isuke iliyopo Halmashauri ya Wilaya Ushetu na kuwataka kutoiga kabisa utamaduni wa nchi nyingene zinazikwenda kinyume na tamaduni zetu watanzania.
Aidha akawata pia wanafunzi wa kiume kuwalinda dada zao, kutowafanyia ukatili wadogo zao au wengine na kujilinda wao wenyewe pia kwani vita ya kupambana na ukatili ni yetu sote hivyo wasikubali kabisa kutokea kwa aina yoyote ile katika maeneo yao wanayoisha.
"Nataka niwaeleze wanangu wote na mnisikilize kwa makini, msikubali kabisa kufà nyiwa ukatili na mtu yoyote, na kama kuna viashiria vyovyote vya ukatili toeni taaeifa mapema kwa wazazi, walezi, walimu, kwa viongozi au kwa ofisi yoyote ya Serikali, nanyi vijana muwalinde dada zenu, wadogo zenu, msiwanyie ukatili na msiache kujilinda ninyi wenyewe pia," alisisitiza Mhe. Mndeme.
Pamoja na kazi nyingine lakini pia Mhe. Mndeme amekagua miradi 6 mbalimbali itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Ushetu huku akimtaka Meneja wa Tarura -Ushetu kurekebisha miundo mbinu ya barabara iweze kupitika kabla, wakati na baada ya Mwenge kupita.
Picha ikonesha sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isuke iliyopo Halmashauri ya Ushetu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao
Moja kati ya Tenki kubwa la maji alilotembelea Mhe. Mndeme mradi unaotekelezwa na RUWASA.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa