MKUU wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 20 Res, 2023 ameunda kamati ndogo yenye lengo la kuiikwamua Timu ya Stand United ambayo inapitia wakayi mgumu ikiwemo kifdha.
RC Mndeme amefikia uamuzi wakati alipokuwa akiongoza kikao cha wadau wa michezo mkoa wa shinyanga ambapo alisikiliza na kupokea maoni ya wadau ambaonkwa kauli moja walishauri umuhimu wa uwepo wa kamati isiyozidi watu watano ambapo kamati itakutana, kujadili na kupendekeza namna ambavyo itakutana na wadau.
Kamati pia itakuwa na wajibu pia wa kujadiliana na wadau na kisha kupeleka mapendekezo kwake kwa lengo la kuivusha timu hii ambayo kwa sasa inasemekana kuwa katika wakati mgumu sana wa kifedha.
"Ndugu zangu wajumbe, nimesikiliza maoni na usari wa wajumbe mbalimbali sasa nitaunda kamati ndogo itakayokuwa na wajib wa kuratibu, kufuatilia na kutekeleza maelekezo ya wadau mbalimbali kwa lengo la ku8nusuru timu yetu, nami nashauri iongozwe na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi", alisema Mhe. Mndeme.
Pamoja na mambo mengine, kamati kwa kauli moja imwridhia kuikwamua timu ya mpira wa miguu ya atand united na kusitisha mambo mengine yahusuyo michezo kwa sasa kwakuwa inapitia wakati mgumu sana.
Kamati iliyoundwa inamjumlisha Mhe. Johari Samizi ambaye ni mkuu wa wilaya ya ahinyanga, Mhe. Elias Masumbuko ambaye ni Mstahiki Meya Manispaa ya ahinyanga, Mhe. Masalu Nyese ambaye ni Diwani Kata ya mwakitolyo, Base Kamanda Shinyanga (JWTZ Kanali Sunzu Machuza na Afisa Michezo mkoa wa shinyanga Bi. Jesca na Benard Mihayo afisa uhusiano Mgodi wa Mwadui.
Awali akimkaribisha Mhe. Mndeme, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo ambaye ndiye wenyekiti wa Michezo mkoa wa shinyanga alimuambia kuwa, wadau wamekusanyika hapa wakiwa na shauku ya kumsikia RC Mndeme juu ya masuala mbalimbali yahusuyo michezo mkoa wa shinyanga ikiwemo Stand United.
Kando na hayo, pia RC Mndeme aliendesha harambee kwa kuanzia ambapo ilipatikana Tzs. MIl. 8.7 huku taslimu ikiwa Mil. 1.6 na nyingine ni ikiwa ni ahadi zilizotolewa na wadau mbalimbali.
Prof. Siza Tumbo, ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa shinyanga akifuatilia mjadala wakati wa kikao
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko wakati wa kikao cha wadau wa michezo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa