Leo tarehe 14 Desemba 2023 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amempoka Mwekezaji mkubwa wa Kiwanda cha Vifaa vya Plastiki cha Kampuni ya MAISHA UNDERTAKING COMPANY LIMITED kilichopo Kibaha, Pwani (Mr Jiwen Yang) kwa lengo la kujitambulisha.
Lakini pia wamekuja na dhamira kuu ya kumfahamisha RC Mndeme kwamba wanatarajia kujenga kikubwa cha kuzalisha bidhaa za plastiki katika eneo la Nhelegani Manispaa ya Shinyanga na Manispaa ya Kahama ambapo bidhaa hizo zitasambazwa katika mkoa wa Shinyanga na mikoa, mikoa yq jirani na mikoa yote ya kanda ya Ziwa na nchi za jirani.
Mwekezaji Mr Jiwen Yang ambaye kampuni yake imepata ardhi yenye ukubwa wa hekta 3 eneo la Nhelegani ambapo atajenga kiwanda na maghala makubwa ya bidhaa hizo, huku akimhakikishia RC Mndeme kuwa ataleta wawekezaji wengi zaidi kutoka nchini China ili wawekeze mkoa wa Shinyanga.
"Nakuahidi Mhe. RC Mndeme kuwa, nimevutiwa sana kuwekeza mkoani kwako hapa shinyanga kwakuwa nimeona siasa ni safi, uongozi borĂ , miundombinu ipo safi na rasilimali za kutosha hapa, hivyo ninawekeza na pia ninakwenda kuwashawishi na wengine waje kuwekeza mkoa aa shinyanga", amesema Mr Jiwen Yang.
Kwa upande wa Mkoa RC Mndeme amesema mwekezaji atapata ardhi zaidi yenye ukubwa wa hekta 20 katika Manispaa ya Shinyanga na hekta zingine 20 katika Manispaa ya Kahama kwakuwa wakurugenzi wamethibitisha hili wakurugenzi hawa waliokuwepo katika kikao cha leo. Asante sana Mhe Christina Mndeme kwa ushirikiano mkubwa uliotupatia leo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa