Na. Paul Kasembo, Shinyanga DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 27 Aprili, 2024 amefika katika kijiji cha Mishepo kilichopo Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kutoa pole kwa waathirika wa mvua zinazoendele huku akimshika mkono wa rambirambi Mzee Ngassa ambaye katika kadhia hii amefiwa na watoto watatu.
Akizungumza na wananchi wa maeneo haya, RC Macha amesema kuwa alipokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizi za maafa na ndiyo sababu akaamua kuja kutoa pole sanjari na kuwataka wakazi hawa kuendelea kuchukua tahadhari zaidi hasa wale wanaoishi maeneo hatarishi ikiwamo ya bondeni.
"Tumefika hapa kwa lengo la kuwapa pole ninyi nyote mliopatwa na maafa haya, ni mipango ya Mwenyezi Mungu lakini nasi tuchukue tahadhari zaidi na kwa wale mliopo maeneo hatarishi niwaombe myapishe maeneo hayo hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha," amesema RC Macha.
Wito watolewa na RC Macha kwa wananchi kuendelea fuatilia na kusikiliza ushauri unaotolewa na wataalam wetu wakiwemo wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambao wamekuwa wakitoa utabiri wa hali ya leo hewa kila siku kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa