BARIADI - SHIMIYU
Mkuu wa Mkoa wa Sinyanga Mhe. Anamringi Macha ameshiriki kikao cha maandalizi ya Sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Bariadi Comference katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Kikao hiki kimefanyika tarehe 5 Julai, 2024 ambacho kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenan Kihongozi pia kimehudhuriwa na Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waratibu wa maonesho pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali.
Baada ya kikao viongozi hawa wametembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyopo Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi
HABARI PICHA
Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenan Kihongosi akiongoza kikao
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga aliyesimama Mhe. Julius Mtatiro wakati wa kikao
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu (wa kwanza kutoka mkono wa kulia) Mhe. Joseph Mkude
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa