• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MACHA AFUNGUA BONANZA LA MICHEZO YA JESHI LA WANANCHI BEZI YA SHINYANGA LA KUAGA MWAKA 2024 NA KUKARIBISHA MWAKA 2025

Posted on: February 7th, 2025

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 7 Februari, 2025 amefungua Bonanza na michezo ya Jeshi la Wananchi Bezi ya Shinyanga la kuaga mwaka 2024 na kukaribisha mwaka 2025.

Pamoja na mambo mengine RC Macha ameipongeza Bezi ya Shinyanga inayoongozwa na Kanali Raphael Faustine Chachankwa kazi nzuri wanayoifanya sanjari na kuandaa michezo hiyo ambayo imewakutanisha askari wa vikosi vyote hapa Shinyanga na kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kati ya Kikosi cha 941 Regt  kilichoungana na 976 Regt dhidi ya Kikosi cha 82 Regt kilichoungana na 516 KJ.

RC Macha amefungua bonanza hilo katika viwanja vya Fresho vilivyopo Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, Mkuu wa Bezi ya Shinyanga Kanali Raphael Faustine Chacha na Maafisa wengine kutoka Bezi ya Shinyanga na kusisitiza kuwa Wanashinyanga na Watanzania kwa ujumla wanajivunia sana uwepo wa jeshi hili la wananchi.

"Pamoja na bonanza hili zuri la michezo, lakini pia ninawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, tunayo amani ya kutosha na utulivu mkubwa nchini kwetu, hakika kwakweli tunajivunia sana uwepo wenu," amesema RC Macha.

Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Kanali Raphael alisema Bezi ya Shinyanga ilianza kwa kutembelea na kutoa misaada mbalimbali ya kiutu kwa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha Lohada kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga huku akisisitiza kuwa Jeshi la Wananchi Bezi ya Shinyanga litaendelea kuandaa bonanza kama hizo kila wakati na kwamba wataendela kumuomba ili aendelee kushiriki nao kila itakapohitajika.

Huu ni utaratibu wa kawaida wa Jeshi la Wananchi Bezi ya Shinyanga wa kuandaa na kushiriki katika Bonanza mbalimbali kwa lengo la kuwakutanisha ili kushiriki michezo mseto ukiachilia mbali hili la leo ambalo lilikuwa maalum kwa lengo la kuaga mwaka 2024 na kukaribisha mwaka 2025.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • NATOA WITO KWA VIJANA HAPA SHINYANGA KUREJEA NA KUTATHIMINI UPYA NJIA ZA KUJIPATIA KIPATO - RC. MACHA

    May 20, 2025
  • SERIKALI YATHIBITISHA VIFO VYA WATU SITA NA MAJERUHI 11 KATIKA AJALI YA MGODI WA MWAKITOLYO.

    May 18, 2025
  • WAZAZI NA WALEZI, NENDENI MKAWE MABALOZI SAHIHI WA KAZI ZA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – RC. MACHA

    May 16, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa