Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amefungua kikao cha kutoa maoni ya kuboresha Mpango Mkakati wa Mkoa awamu ya pili wa Kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto huku akiwataka wajumbe kujadili kwa kina na kwa maslahi mapana ya walio wengi ambao tunawawakilisha hapa.
CP Hamduni amefungua na kuyasema haya leo tarehe 30 Septemba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo Bi. Joyce David Kessy kutoka Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) ambalo makao makuu yake yapo Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho Bi Joyce amesema, maboresho hayo ya mpango mkakati wa Mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto yanafanyika kupitia mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU unaotekelezwa na Shirika la WiLDAF kwa kushirikiana na UNFPA chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa