Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Msaidizi, Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dafroza Ndalichako amefungua Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata tarehe 29 Novemba, 2023 Mkoani Shinyanga.
Akifungua mafuzo haya kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo Mwl. Ndalichako ametoa wito kwa Maafisa hao kuhakikisha wanayachukua na kuyazingatia yale yote wanayofundishwa na sio kuyacha wakitoka hapo sababu mafunzo hayo yatawaongezea maarifa na ujuzi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amewataka kujua na kukumbuka wao ni viongozi sahihi na kuchaguliwa kwao hakujakuwa kwa bahati mbaya bali walionekana wanaweza kuisaidia Serikali katika kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wake.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Hamisi Mkunga amesema, kama Wizara inavyofanya kazi na wananchi wake moja moja itaendelea kusimamia maadili ya watumishi wa umma inayowasimamia na pia kuhakikisha watumishi hao wanajengewa uwezo na kupewa mafunzo kwa ajili ya kuwa waadilifu, waaminifu na wabunifu katika maeneo yao ya kazi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa