Na. Paul Kasembo, KISHAPU
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka watumishi wa Wilaya ya Kishapu kuhakikisha wanaongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali bila kubughudhi wafanyabiara na wananchi katika maeneo yao ya kazi ili kuwezesha utekelezaji wa miradi yenye tija kwa muktadha wa maisha wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema Mhe. Macha wakati akizungumza na watumishi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Kishapu ambapo pamoja na maelekezo mengine ameitaka TARURA Wilaya ya Kishapu kuhakikisha wanafanya usafi katika mifereji yote iliyojengelewa ili kuufanya mji kuwa safi na kutunza mazingira.
"Nendeni mkaongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali bila kubughudhi wafanyabiashara na wananchi ili waweze kuwa tayari kulipa ambapo mapato haya yataiwezssha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo itakayokuwa na tija kwao," amesema RC Macha.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa