SHINYANGA.
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Patrobasi Katambi kwa niaba ya Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB), amesema kuwa vyombo vya habari ni lazima viwe na wakalimani wa lugha ya alama ili kuwawezesha watu wasioweza kusikia kupata haki yao stahiki ya kuhabarishwa kama ilivyo kwa watu wengine.
Mhe. Katambi amesisitiza kuwa hatua mbalimbali zilizofikiwa na Serikali katika Chmacha cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimeadhimisha Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani ambapo Kitaifa yamefanyika katika Mikoa wa Shinyanga iliyobeba kauli mbiu isemayo 'Ungana kutetea Lugha ya alama'.
Hayo yamesemwa leo tarehe 28 Septemba, 2024 katika wakati akihutubia halaiki hii ambayo ambayo imefanyika katika viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga hapa mkoani Shinyanga,
Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania na mjumbe wa Chama cha Viziwi Tanzania CHAVITA Mkoa wa Dar es salaam Bi. Tungi Mwanjara Kwa niaba ya viziwi ameiomba serikali kuajili wakalimani kwenye taasisi za umma na vyombo vya habari Ili kusaidia watu wasiosikia kupata taarifa kamili na muhimu zinazoendelea nchini na Dunia nzima.
"Wakati umefika sasa kwa vyombo vya habari kuwa ba wakalimani wa lugha ya alama ili kuwawezesha watu wasioweza kusikia kupata haki yao stahiki ya kuhabarishwa kama ilivyo kwa watu wengine, amesema Mhe. Katambi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania na mjumbe wa Chama cha Viziwi Tanzania CHAVITA Mkoa wa Dar es salaam Bi. Tungi Mwanjara Kwa niaba ya viziwi ameiomba serikali kuajili wakalimani kwenye taasisi za umma na vyombo vya habari Ili kusaidia watu wasiosikia kupata taarifa kamili na muhimu zinazoendelea nchini na Dunia nzima.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa