Mamlaka ya Majisafina Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetoa taarifa yake ya utekelezaji wa majukumu yake katika kuwahudumia wananchi wake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 huku ikiahidi maboresho makubwa zaidi Tinde, Didia, Shinyanga Manispaa na Iselamagazi.
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka CPA. Sarah Emmanuel amesema kuwa kwa sasa SHUWASA inatoa huduma kwa wakazi 282,698 lakini waliofikiwa na huduma ya majisafi moja kwa moja kupitia maunganisho ya majumbani na magati kww maeneo yote yanayohudumiwa na Mamlaka ni wakazi 186,580.
"Ndugu waandishi wa habari kwa ujumla mahitaji ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga na miji midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi ni mita za ujazo 18,833 kwa siku, ambapo kwa mwezi Mei 2023 Mamlaka ilisambaza maji yenye mita za ujazo 417, 977 sawa na wastani wa mita za ujazo 13,483,1 kwa siku na kati ya maji hayo 18.6% yalipotea kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kupasuka mabomba na njia nyingine zisizo rasmi," alisema CPA. Sarah.
SHUWASA inatekeleza miradi minne (4) midogo ndani ya eneo la Manispaa ya Shinyanga yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.6 fedha toka Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji ambapo kwa eneo la Tinde Mamlaka inasambaza mtandao wa maji Kilomita 8.1 kwa awamu ya kwanza ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ujenzi wa mradi wa Tinde-Shelui.
Eneo jingine ni Didia ambako Mamlaka inasambaza mtandao wa maji Kilomita 8.1 (KM 1.9 bomba kuu na KM 6.2 bomba za usambazaji) ambao upo 62% na unatarajiwa kukamilika Julai, 2023 ambapo Didia pia panajengwa Tangi la maji lenye ujazo wa mita za ujazo 100 ni mradi ambao upo katika hatua za majaribio.
Iselamagazi ni moja ya eneo linalohudumiwa na Mamlaka ambapo zaidi ya Milioni 106 zimetengwa kwa ujenzi wa mtandao wa bomba za usambazaji KM 3.14 fedha kutoka Mfuko wa Maji ikiwa zaidi ya Milioni 31 zimepokelewa na Mamlaka na kuanza ujenzi wa KM 1.75 unaotarajiwa kukamilika Julai 2023 na kumufaisha wakazi zaidi ya 3000.
SHUWASA na SHIRIKA LA MAENDELEO LA UFARANSA (AFD) inatekeleza mradi mkubwa wenye thamani ya EURO 76 uliosainiwa Juni 20, 2022 ambapo SHUWASA kupitia Wizara ya Fedha imepokea EURO 10 na Zabuni mbili za Wahandisi Washauri pamoja na Usaidizi wa Mamlaka zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Aidha SHUWASA haijaanza kutoa huduma ya MAJITAKA wal uondoaji wa majitaka, hata hivyo inachakata TOPE KINYESI kwa kushirikiana na Manispaa ya Shinyanga kupitia mtambo uliopo Kata ya Kizumbi uliojengwa kwa ufadhiri wa SNV.
Pamoja na ufanisi huu mzuri lakini SHUWASA pia inakabiliwa na changamoyo kadhaa ikiwamo uchakavu wa miundombinu, wadaiwa wakubwa kutolipa madeni lakini imejipanga kuboresha huduma kwa wateja wake wa Manispaa ya Shinyanga, Mji mdogo wa Tinde, Didia na Iselamagazi, kuendelea kutoa elimu kwa umma nk.
Kwa ujumla Mamlaka inayo vyanzo vyake vikuu vya maji vitatu (3) ambavyo ni 1. Visima virefu (Bushora na Tinde 2. Bwawa la Ning'hwa na 3. Maji ya Ziwa Victoria.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa