Na. Shinyanga RS.
KAMATI ya Kudumu ya Bhnge ya Miundombinu inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Selemani Moshi Kakoso imeipongeza sana Serikali kupitia ujnezi wa Mkongo wa Taifa ambapo leo Kamati imetembelea na kukagua kituo cha Mkongo uliopo TTCL - Shinyanga kwa niaba ya vituo vingine 32 uliogharimu zaidi ya Bilioni 1 unazozalisha 800G unaohudumia Singida - Shinyanga - Mwanza, Shinyanga Kahama huku Kamati ikiishauri Serikali kuwa imefika wakati TTCL ijiendeshe kibiashara na iweze kuisaidia serikali katika kupunguza gharama za uendeshaji.
Pongezi hizi zinetolewa leo tarehe 14 Machi, 2024 ambapo Kamati imetembelea na kushuhudia namna ambavyo Mkongo wa Taifa unavyofanya kazi katika Kituo cha TTCL Mkoa wa Shinyanga ambapo taarifa imesemwa kuwa ujenzi huu umejikita katika maeneo makuu mawili ambayo ni Usimikaji wa Mitambo ya ujenzi wa nguzo za zege sambamba na utaji wa Waya za Faiba huku taarifa ikionesha kuongezeka kwa uwezo kutoka 200G hadi 800G.
"Kwa niaba ya Kamati, nipende kuwapongeza sana Serikali katika utekelezaji wa ujenzi wa mtandao wa mawasiliano kati ya Mikoa yetu na sas mmevuka nje ya Nchi kwa lengo la kurahisisha mawasiliano na kuileta dunia pamoja, ushauri wetu kwenu, ifike wakati sasa TTCL ije na ubunifu utakaowezesha kujitegemea, kujiendesha kibiashara ili kuipunguzia mzigo Serikali kwa kuwa hivi sasa inatoa huduma mpaka nje ya Nchi," amesema Mhe. Kakoso.
Akizungumza wakati wa ziara hii Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) kwanza amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara na taasisi zake kifedha ilimkuweza kuboresha huduma kwa wananchi kama inavyoshuhudiwa leo kupitia Mkongo huu wa Taifa.
Mhe. Nape amesema, kwa ujumla juhudi kubwa zimefanywa na Serikali katika kuhuisha na kuboresha utoaji huduma ambao ameusema kuwa Mkongo wa Taifa ni barabara ya mawasiliano inayoiunganisha Nchi ndani na nje huku akisema bado kuna baadhi ya jamii haijaingia kwenye mfumo wa simu janja lakini kwa ujumla wamepokea pongezi, ushauri na maelekezo yote na watayafanyia kazi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa