Na. Shinyanga RS.
BARRICK Mgodi wa Barrick bulyanhulu kwa kushirikiana na kampuni ambayo ni mzabuni ndani ya mgodi huo Kakola Digital Solution wamegawa miche ya miti 500 aina mbalimbali katika shule mpya ya msingi ya bulyanhulu iliyopo kata ya bulyanhulu Halmashauri ya Msalala wilaya ya kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza Baada ya kukabidhi miche hiyo Mkurugenzi wa Kakola Digital Solution David Semwenda Amesema wameamua kushirikiana na mgodi kutoa miche hiyo ya miti ikiwa ni kurudisha shukrani kwa jamii inayozunguka mgodi lakini ikiwa wao wanufaika na mgodi kwa kuwa wazabuni lazima warudishe kidogo wanachopata ili jamii ijivunie kuwa na kampuni za wazawa walioaminiwa na wawekezaji.
“ Tunaushukuru sana mgodi wa barrack bulyanhulu kwa kutuamini kama vijana wazawa na kukubali kufanya kazi na sisi lakini pia kulingana na mazingira ya shule hii ni mpya na haikuwa na miti yoyote hivyo tukaona tuanze na shule hii kisha tutaendelea na shule nyingine” david alisema
Aidha kwa mkuu wa shule hiyo Bi.Joyce Lwanji Amesema wanaishukuru sana kampuni ya kakola digital pamoja na mgodi wa barrack bulyanhulu kwa kuwapatia miche hiyo huku akiahidi kuwa wataitunza miti hiyo ili kuwapa Imani na wadau wengine kuendelea kufadhili vitu mbalimbali katika shule hiyo.
Kwa Upande wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia mwakilishi wao Marry Lupamba Amesema Mgodi utaendelea kushirikiana na Serikali na Wadau mbalimbali katika kuwaletea maendelea wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi huo ili tu nao wanufaike na uwekezaji uliowekwa nchini.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa