Mkoa wa Shinyanga ulikuwa ni sehemu ya Mkoa wa Ziwa (Lake Province) mpaka mwaka 1963 ulipoanzishwa rasmi ukiwa na Wilaya tatu (3) ambazo ni Maswa, Shinyanga na Kahama iliyomegwa kutoka Mkoa wa Tabora. Kuanzia Mwaka 1972 hadi mwaka 1982 Serikali ya Mkoa ilikuwa katika mfumo wa Madaraka Mikoani ambapo vyama vya ushirika, utemi na Serikali za Mitaa zilifutwa. Mkoa uliongozwa na Mkuu wa Mkoa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (Regional Development Director) ambaye alisimamia wakuu wa idara mbalimbali. Muundo huu wa utawala ulitumika hadi mwaka 1997 ambapo ulibadilishwa kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa (Regional Administration Act No. 19 of 1997). Sheria hiyo ilifuta cheo cha Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa na kuanzisha cheo cha Katibu Tawala Mkoa. Katibu Tawala Mkoa ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali katika Mkoa.
Mkoa wa Shinyanga uliendelea kukua ambapo maeneo mapya ya Utawala yalianzishwa na kufikia Wilaya saba ambazo ni Kahama, Bukombe, Maswa, Kishapu, Bariadi, Meatu na Shinyanga. Aidha kuanzia mwaka 2012 kutokana na Mkoa kukidhi vigezo muhimu vya kitaifa vya uanzishaji maeneo mapya ya utawala, Serikali ilifanya uamuzi wa kuanzisha maeneo mapya ya Utawala ambapo Mikoa mipya ya Simiyu na Geita ilianzishwa ikiwa imemega baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Shinyanga. Wilaya za Bariadi, Maswa na Meatu zilimegwa kuanzisha Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Bukombe ilipelekwa Mkoa mpya wa Geita. Aidha, Mkoa wa Shinyanga uliongeza maeneo ya Kiutawala kwa kuanzisha Halmashauri mpya za Kahama mji mwaka 2012, Msalala na Ushetu mwaka 2013 ambazo zilitokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Kahama. Uamuzi huu wa Serikali unalenga kuboresha huduma za kiutawala na maendeleo ili wananchi waweze kuzipata kwa karibu zaidi. Jedwali lifuatalo linaloonesha Mgawanyo wa Mkoa kiutawala kwa sasa.
Mgawanyo wa Mkoa wa Shinyanga Kiutawala
Wilaya |
Halmashauri |
Ukubwa wa eneo (km2)
|
Tarafa |
Kata |
Vijiji |
Mitaa |
||
1
|
Kahama
|
1
|
Manispaa ya Kahama
|
1,515 |
2 |
20 |
45 |
32 |
2
|
Ushetu
|
5,311 |
2 |
20 |
112 |
- |
||
3
|
Msalala
|
2,637 |
1 |
18 |
92 |
- |
||
2
|
Kishapu
|
4
|
Kishapu
|
4,334 |
3 |
25 |
117 |
- |
3
|
Shinyanga
|
5
|
Shinyanga
|
4,212 |
3 |
26 |
126 |
- |
6
|
Manispaa ya Shinyanga
|
548 |
3 |
17 |
19 |
55 |
||
Jumla
|
18,555 |
14 |
126 |
511 |
87 |
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Machi 2017
Mipaka ya Mkoa:
Mkoa wa Shinyanga uko Kaskazini – Magharibi mwa Tanzania na Kusini mwa Ziwa Victoria. Mkoa unapakana na Mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita kwa upande wa Kaskazini, upande wa Mashariki Mkoa wa Simiyu, Upande wa Magharibi Mkoa wa Geita upande wa Kusini Mkoa wa Tabora. Mkoa uko kati ya nyuzi za Latitudo 30 12’ - 40 27’ Kusini mwa Ikweta na nyuzi za Longitudo 310 29’ - 340 18’ Mashariki ya Greenwich. Mkoa wa Shinyanga una eneo la kilometa za mraba 18,555..
RAMANI YA MKOA WA SHINYANGA KIUTAWALA
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Machi, 2017
3.0.1 UONGOZI WA MKOA
Mkoa wa Shinyanga umeongozwa na wakuu wa mikoa 24 tangu mwaka 1963 kama orodha inavyoonesha hapa chini:
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa