Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 utawasili Mkoani Shinyanga tarehe 08 Mei, 2019. Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatafanyika katika kijiji cha Namba tisa Kakola, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kukimbizwa kwenye Halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga.
Ratiba ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga ni kama ifuatavyo:-
Tarehe 08 Mei, 2019 – Halmashauri ya Wilaya ya Msalala (Mwenge utapokelewa kutoka Mkoa wa Geita)
Tarehe 09 Mei, 2019 – Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Tarehe 10 Mei, 2019 – Halmashauri ya Mji Kahama
Tarehe 11 Mei, 2019 – Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Tarehe 12 Mei, 2019 – Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Tarehe 13 Mei, 2019 – Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Kauli mbiu ya mbio za Mwenge mwaka huu ni “MAJI NI HAKI YA KILA MTU, TUVITUNZE VYANZO VYAKE NA TUKUMBUKE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA”
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa