Baada ya kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Brg. Gen. Yohana Balele siku ya tarehe 30/03/2009, Mheshimiwa Stephen Wasira aliendelea na Ziara yake katika Mkoa kwa kutembelea wilaya mbali mbali za mkoa. Waziri Wasira alikagua shughuli mbali mbali za kilimo zinavyofanyika mkoani Shinyanga ikiwa ni pamoja na kufungua ghala la chakula na kutembelea shamba la pamba kama anavyoonekana katika picha. |